Kila mwaka, kuzinduliwa kwa Muhtasari wa Kibinadamu Ulimwenguni ni fursa ya kuangazia ni wapi mahitaji ni makubwa zaidi - na ni kiasi gani cha fedha kinachohitajika kusaidia baadhi ya watu walio hatarini zaidi duniani. Tutakuwa tunakuletea habari kutoka kwa matukio yanayoendelea Kuwait, Nairobi na Geneva, yakisimamiwa na Mratibu mpya wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Dharura Tom Fletcher. Watumiaji wa programu ya UN News wanaweza kufuata hapa.