Clementine Nkweta-Salami alisema Mlipuko wa hivi punde wa uhasama katika mji mkuu wa Kordofan Kusini, Kadugli, umeripotiwa kupoteza maisha ya raia 80 na kuwaacha wengine wengi kujeruhiwa.
Alilaani matumizi yaliyoripotiwa ya wanawake na watoto kama ngao za binadamu huko, pamoja na kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu na kuwekwa kizuizini kwa raia wakiwemo watoto.
Mahitaji ya kibinadamu pia yanasalia kuwa muhimu huko Blue Nile, ambapo tishio la ghasia na ripoti za uhamasishaji wa watu wengi kwa vita tena vinahatarisha vurugu zaidi.
Migogoro ya kina zaidi inanyemelea
Ukosefu wa usalama unaozidi unatishia kutumbukiza majimbo yote mawili kwenye mzozo mkubwa zaidi, kulingana na afisa wa juu wa misaada.
Alisema kuwa kwa muda mrefu, raia wameshindwa kupata msaada wa kuokoa maisha na huduma za kimsingi kutokana na ukosefu mkubwa wa vifaa vya matibabu, upatikanaji mdogo wa kibinadamu na migogoro inayoendelea.
"Huu ni wakati muhimu, kwani matokeo ya uhaba wa chakula tayari yanaonekana katika sehemu za Kordofan Kusini, ambapo familia zinanusurika kwa kutegemea chakula kidogo, na viwango vya utapiamlo vinaongezeka sana,” alisisitiza.
Zaidi watateseka
Bi Nkweta-Salami alionya kwamba ikiwa mapigano yataendelea, watu wengi zaidi wataachwa bila kupata msaada muhimu, mateso ya wanadamu yataongezeka, na maisha zaidi yatapotea.
Jeshi la Sudan na wapinzani wa kijeshi wa Rapid Support Forces (RSF) wamekuwa katika mapigano makali ya kutaka kudhibiti nchi ya tatu kwa ukubwa barani Afrika tangu Aprili 2023.
Bi. Nkweta-Salami alitoa wito kwa pande zote katika mzozo huo kupunguza hali ya wasiwasi, kulinda raia na miundombinu ya kiraia, na kuruhusu wahudumu wa kibinadamu kuwafikia wale wanaohitaji bila vikwazo.