Hakuna msaada wowote ulioingia katika eneo hilo tangu Israel ilipotekeleza marufuku hiyo tarehe 2 Machi na watu wote, zaidi ya watu milioni mbili, wako katika hatari ya njaa.
"Kama tulivyoonyesha wakati wa usitishaji mapigano mwaka huu - na kila wakati tumepewa ufikiaji - Umoja wa Mataifa na washirika wetu wa kibinadamu wana utaalamu, azimio na uwazi wa kimaadili kutoa misaada kwa kiwango kinachohitajika kuokoa maisha kote Gaza," alisema Bw. Fletcher.
Tayari kusonga
Wale wanaopendekeza njia mbadala ya usambazaji wa misaada hawapaswi kupoteza muda, aliongeza, kama mpango tayari ipo.
Hati hiyo "imejikita katika kanuni zisizoweza kujadiliwa za ubinadamu, kutopendelea, kutoegemea upande wowote na uhuru." Zaidi ya hayo, inaungwa mkono na muungano wa wafadhili, pamoja na wengi wa jumuiya ya kimataifa, na iko tayari kuanzishwa ikiwa wasaidizi wa kibinadamu wataruhusiwa kufanya kazi zao.
"Tuna watu. Tuna mitandao ya usambazaji. Tuna imani ya jumuiya mashinani. Na tunayo misaada yenyewe - pallet 160,000 - tayari kuhama. Sasa," alisema.
'Tufanye kazi'
Bw. Fletcher alikariri kwamba jumuiya ya kibinadamu imefanya hivi hapo awali na inaweza kufanya hivyo tena.
"Tunajua jinsi ya kusajili vifaa vyetu vya msaada, kuchunguzwa, kukaguliwa, kupakiwa, kupakuliwa, kukaguliwa tena, kupakiwa tena, kusafirishwa, kuhifadhiwa, kulindwa dhidi ya uporaji, kufuatiliwa, kubebwa na lori, kufuatiliwa na kuwasilishwa - bila kukengeushwa, bila kuchelewa, na kwa heshima. Tunajua jinsi ya kuwafikia raia walio na uhitaji mkubwa na kuzuia njaa."
Alihitimisha taarifa hiyo kwa kusema "Inatosha. Tunadai utoaji wa msaada wa haraka, salama na usiozuiliwa kwa raia wanaohitaji. Tufanye kazi."