Tunakumbuka kwa muhtasari picha nzuri zaidi za siku ya tatu ya ziara ya kihistoria ya Papa nchini Iraq.
Baba Mtakatifu Jumapili alitembelea miji ya Erbil, Mosul na Qaraqosh, ambako alirudia wito wake wa udugu, matumaini na amani.
Papa Francis alianza siku hiyo mjini Erbil, ambako alikutana na Rais na Waziri Mkuu wa eneo linalojiendesha la Kurdistan ya Iraq, pamoja na mamlaka za kiraia na kidini.
Kutoka Erbil, Papa Francis alisafiri hadi Mosul, ambapo, katikati ya uharibifu uliofanywa na ISIS, aliombea amani kwa wahasiriwa wa vita nchini Iraq na Mashariki ya Kati.
Katika Kanisa la Immaculate Conception, katika mji wa Qaraosh, kaskazini mwa Iraq, Papa alikutana na wakristo wa eneo hilo, akiwataka kujenga upya jumuiya zao kwa msingi wa msamaha na udugu.
Hatimaye, Papa Francis alirejea Erbil, ambako aliadhimisha Misa ya Jumapili na waamini wapatao 10,000.
"Leo," alisema katika mahubiri yake, "naweza kuona kwanza kwamba Kanisa katika Iraqi liko hai, na kwamba Kristo yu hai na anafanya kazi katika hili, watu Wake watakatifu na waaminifu,"