Wakati zaidi ya robo tatu ya watu wazima wote wanaoishi na VVU wanapokea aina fulani ya matibabu, idadi ya watoto wanaofanya hivyo, inafikia asilimia 52 pekee. Katika kukabiliana na tofauti hii ya kushangaza, mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNAIDS, UNICEF, WHO, na mengine, yameunda muungano wa kimataifa ili kuzuia maambukizi mapya ya VVU na kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 watoto wote walio na VVU wanaweza kupata matibabu ya kuokoa maisha.